Karibu hapa Tutunata

Katika blog hii tutazungumzia mahusiano na mafanikio.
Tutachambua mbinu na mikakati ya namna ya kupiga hatua kila siku toka sehemu moja ya chini kwenda juu zaidi. Utaweza kujiongeza na kupata matumaini mapya ya maisha.

Smiley face

Thursday, May 10, 2018

JINSI YA KUWA MTU MWENYE KUJIAMINI

No comments:
Kutokujiamini ni janga kubwa kwa mtu binafsi na kwa wale wanaomtegemea. Kutokujiamini kunakufanya ushindwe kupiga hatua katika Maisha yako na wakati mwingine usiwe mtu mwenye furaha. Kutokujiamini hutokea katika maeneo mbalimbali iwe kwenye elimu, kazi , mahusiano, biashara, na hata malezi. 
Ili kupambana na kutokujiami na wewe uanze kuwa mtu wa kujiamini  inakupasa kwanza ujue kwanini haujiamini. Hivyo tuangalie sababu zifuatazo za kitaalamu kwa nini watu hupoteza kujiamini:
1.Kutokua na Uhakika wa namna ya kufanya  jambo husika: Unapokosa taarifa sahihi kuhusu kile ukifanyacho au kushindwa kuchanganua mambo vizuri utaanza kujitilia mashaka wewe mwenyewe na hivyo utashindwa kulifanya jambo husika.
Mfano kama hujui vema miundo ya sentensi za Kiingereza, huzijui kanuni na maneno ya English, utakapohitajika kuongea au kuandika kitu kilichonyooka, wewe mwenyewe utaanza kujitilia mashaka, uoga utaingia na utakosa kujiamini.
DAWA YAKE: Dawa ya kutokujiamini kwa sababu  huna uhakika na namna ya kufanya jambo ni kuhakikisha tuu unapata taarifa na ujuzi sahihi. Tafuta kujifunza na sana sana upate mtu atakayekuongoza na kusimamia maendeleo yako ya karibu ili akupe mrejesho vile unavyoendelea katika kujiboresha.
La kusisitiza hapa ni kuwa uwe tayari kupata ujuzi na kujiboresha ili uweze kujiamini kweli kweli.
2. Yaliyokutokea zamani kuhusu kushindwa jambo husika:
Wakati mwingine ni sehemu ya ubongo wako inayohifadhi mambo yaliyokutokea hapo awali ndiyo inayokufanya ukose kujiamini. Kumbukumbu ya wewe kushindwa jambo Fulani au kuabika kuhusu jambo hilo kunaweza kukupelekea kujitilia mashaka uwezo wako wa kulifanya hilo jambo sasa. Matokeo yake ni kutokujiamini.
DAWA YAKE: Jiboreshe ufahamu wako kuhusu Maisha kwa ujumla. Fahamu kuwa yaliyokutokea mwanzo sio lazima yakutokee tena. Muda umepita na wewe umekua mtu mpya, hivyo kushindwa mwanzoni kusikufanye ujione uliyeshindwa au utakayeshindwa siku zote. Angalia maboresho katika Maisha yako ambayo tayari umeyafanya. Jipe moyo na mtegemee Mungu ili uwe na uthubutu wa kufanya tena ukiwa mtu mpya na bora Zaidi.
3.Kutokua na maandilizi na maboresho ya mara kwa mara:
Kuna wakati hata lile jambo ulilowahi kulifanya hapo kabla na ukaliweza, inakutokea eti leo haujiamini kuwa utaweza kulifanya. Hii inatokana na maandalizi na kutokujifanyia maboresho ya mara kwa mara. Kujiamini ni jambo ambalo linahitaji kulelewa na hivyo basi jizoeshe kujiboresha mara kwa mara. Kkiama ilivyo kiota kinachojengwa kwenye tawi dhaifu, hakitokuwa bora, hivyo hivyo nawe usipokuwa na maandilizi na maboresho mazuri utakosa kujiamini.
DAWA YAKE: Kama kutokujiamini kwako kunatokana na kushindwa kujiboresha vema, basi jiwekee mkakati sasa wa kujiboresha katika yale ambayo ulishawahi kufanya kabla. Maandalizi bora ni muhimu hata kwenye kuongea mbele za watu tunasisitizwa sana kufanya maandalizi kabla ya kuenda kuongea mbele za watu.
4. Kujilanganisha na wengine na ushindani usio na lazima
Ni ukweli ulio wazi kuwa sote tunaishi au tulipo sivyo ambavyo tulitarajia au kutazamia miaka 10 iliyopita. Hii ina maana kuwa mambo hubadilika mara kwa mara na hakuna bingwa wa Maisha. Hivyo basi acha kujilinganisha na kujishindanisha na watu wengine.
Kujilinganisha na wengine na kutaka ushindani na watu vinatajwa kuwa ni adui wakuu wa kujiamini. Inawezekana kwa mfano hata kuongea Kiingereza unashindwa kujiamini kisa tuu unafikiria utakachoongea hakitokua bora kama cha Fulani. Unajilazimisha uongee kama mmarekani. Umejibadilisha sauti ili uongee sijui kama mdada gani mtangazaji wa redio.
DAWA YAKE: Ishi Maisha yakow ewe kama wewe. Kama ni kujiweka bora au kufanya jambo Fulani lifanye kwakua wewe kama wewe unataka hilo na sio kwa sababu wengine wanataka au unataka kuwakomesha au kuwalingishia wengine.
Ni kweli kuwa unapaswa kuwaangalia wengine wanafanya nini na wanajiboreshaje, lakini isiwe kwakua unataka kuwa kama wao au kuwapita maana haujui wao kwanini wanafanya wanayoyafanya, na wala hujui wapo katika hali gani ya Maisha. Isitoshe wewe unachokiona ni kile cha nje tuu, hujui wanapitia nini katika Maisha yao halisi.
5.Kujitegemeza Kupita Kiasi
Unapojiruhusu kusubiri kufanyiwa mambo mengi au kumuangalia mtu Fulani kama ndio mwenye uwezo wa kulifanya jambo matokeo yake ni kuwa wewe mwenyewe unajishusha chini, na mwisho wa siku ni kujiona wewe kama wewe hauna uwezo wa kufanya mambo kwa ufanisi nah apo ndipo kutokujiamini hutokea.
DAWA YAKE: Dawa ya kutokujiamini kwa sababu unamtegemea sana mtu ni wewe mwenyewe kuanza sasa kupenda kujifunza vitu na kuvifanya. Usipende urahisi rahisi, au kuwa mvivu kwakua yupo anayeweza kukufanyia mambo hata kama ni mpenzi wako au mtoto wako.
Watu wengi wamejisahau sana utakuta mambo mengi ni marahisi ila eti mpaka baba arudi, au mpaka mtoto aje amfanyie. Na sio kwamba hawezi ila keshajiona yeye keshapoteza kujiamini kwakua kaegemea sana katika kusubiri wengine wafanye.
6. Mazingira na watu ulionao karibu
Watu ulionao karibu au mazingira uliyomo yanaweza pia kukufanya ukakosa kujiamini. Kuna watu wao hupenda kukosoa sana na kuwafanya wengine walionao karibu wajione hawawezi. Watu hawa wanaweza kuwa hata wazazi, wapenzi wetu, mabosi wetu wengine mashoga na marafiki zetu.
Mazingira uliyopo pia yanaweza kukutengenezea viwango vya namna ya kuishi, au kukutengenezea matarajio fulani kiasi kwamba nawe ukijiangalia ni kama vile haujafikia viwango hivyo au unajiona huwezi kufikia.  Hii inaweza kutokea hata kwa mfano  yale unayosikia kuhusu kuishi na mpenzi wako. Nawe ukapoteza kujiamini mbele ya mpenzi wako kisa tuu wengine wameongelea mambo makubwa ambayo wanayofanya ambayo wewe kama wewe unahisi huwezi kufanya.
DAWA YAKE: Kaa mbali na watu ambao wanajiona wao ndio wajuaji na hawakupi moyo wa wewe kama wewe kufanya vile uwezavyo.
Kuwa makini na makundi , pamoja na utakachosikia mwisho wa siku fahamu wewe unayo Maisha yako na una misingi yako ya Maisha, na kwamba sio lazima ufanye yale ambayo wengine hufanya.
Continue Reading...

Sunday, April 29, 2018

AKILI UNAYOHITAJI WAKATI UPITAPO KWENYE SHIDA .

No comments:


Kuna wakati unaweza kuwa unapitia  magumu ambayo hakuna anayejua ila  wewe na moyo wako tu, hali hiyo inakufanya  wakati mwingine usiwe mwenye furaha ,unakuwa  na hasira kila wakati ,hujiamini,umwamini mtu  ukiona watu wanacheka unahisi unachekwa wewe.

*Inawezekana kinachokunyima amani  ni ndoa,kukosa kazi,watoto, mchumba,biashara haina faida,kodi ya nyumba,masomo magumu ,magonjwa ,bosi mkorofi au huduma unayofanya kanisani au msikitini.

*Hicho ni kipande kidogo  tu kwenye maisha nacho kitapita,usifikiri hali  hiyo unayopitia unapitia   mwenyewe ,ni wengi  wanapitia magumu  tena labda makubwa kuliko yako.

*Tunatofautiana katika  kupokea mambo wapo wanaopitia magumu  maishani  kuliko yako ,lakini wameyapokea kawaida wana amani na maisha yanaenda.

*Vile utapokea tatizo na kuamua kulikuza kuona tatizo ni kubwa kuliko wewe na  lina  akili kuliko wewe ndivyo litakavyokuwa wakati mwingine unafikiri  labda hilo  tatizo ni jipya hakuna anayepitia  tatizo kama hilo. Kumbe ni vile tu watu hawasemi .

*Acha kuruhusu  matatizo yakuongoze na kukutawala,Acha kumwambia kila mtu matatizo yako na uwache kujidanganya kwamba una shida kuliko watu wengine.

*Mungu amempa kila mtu  akili na uwezo wa kufanya mambo,ndio tunaona vitabu vya dini vinasema Mungu alimuumba Adamu na Eva lakini hakuna mahali vitabu  vinasema Mungu akawatengenezea nyumba alijua amewapa akili ya kuwatosha kufanya mambo na alijua wakinyeshewa na mvua watatumia akili kutafuta njia ya kujikinga  ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba.

*Acha kuhuzunika mambo unayopitia ni ya kawaida  tumia tu akili yako kufikiri namna unaweza kutatua tatizo lako ukishindwa tafuta wataalamu au watu unaowaona wamefanikiwa katika hilo jambo kutaka ushauri kwao.

*Pia achana na watu watu ambao kila wakati wanasema mambo ni magumu na hayawezekani, kwani kila jambo unalopitia  ni size yako unaweza kulitatua ......siunajua mti hulala pale ulipoangukia .... na tatizo ulilonalo unaliweza ndiyo maana limekupata wewe na siyo mwingine. Matatizo tunayopitia maishani yanatufanya  tuwe imara zaidi , wewe  shahidi hakuna mtoto wa darasa la pili anayepewa mtihani wa darasa la saba  ni kitu kisichowezekana  ni lazima atapewa mtihani wa kiwango chake alichofikia.

*Pambana kutafuta njia ya kutatua  tatizo ulilo nalo usiridhike na kubakia kusema tuu umeshazoea
-Maisha ndivyo yalivyo,  au wakati mwingine una acha kutatua tatizo linalokusumbua na unaanza kulaumu.mfano:
-Wazazi,
-Serikali ,
-Mume/mke,
-Watoto au kujihukumu mwenyewe.

  SAFARI  YA MAFANIKIONI NI SAFARI AMBAYO KILA  MTU ALIYE HAI INAMHUSU  VIKWAZO NI VINGI NJIANI PAMBANA KUVISHINDA MAANA  VIKWAZO VINAINUKA KUTAKA KUKUCHELEWESHA UFIKE KWA KUCHELEWA  NA UKATE TAMAA UAMUE KUBAKI HAPO AU URUDI ULIKOTOKA .

Continue Reading...

Thursday, April 26, 2018

UKIFANYA HIVI UTAISHI KWA HASARA.

No comments:


Kuna watu wanaishi na mpaka watakufa hawajawahi kuishi maisha yao halisi mengi wanayoishi ni ya kuigiza,kuiga,unafiki,kujionyesha na kujifanya wapo  sawa na wanajali zaidi wengine mpaka wanasahau yaliyo ya muhimu  kwao.

*Vizuri kwenda na wakati ila  jaribu  kuangalia jambo hilo  linakusaidia?
-Je  usipolifanya utapungukiwa na nini?
-Je  lina  umuhimu kiasi gani maishani mwako?

*Usifanye kitu sababu wengi wanafanya ili hali  hawajui mwisho wake .
-Usifanye sababu kuna  mtu maarufu anafanya hivyo.
-Usifanye sababu unataka kuwa maarufu umaarufu hautafutwi huwa unakuja wenyewe kwa kutumia ule  uwezo ambao Mungu ameweka ndani yako.

*Kuna  watu wanafanya mambo kwa kuiga mpaka wanatia huruma ili tu waonekane na wao wanafanya kama wengine hata kama hawafurahii wanachofanya hali  hiyo huitwa (unafiki)
- Wengine wanaona wasipokubaliana na mambo yanayoendelea wataonekana siyo wakisasa na labda watakosa marafiki.
-Kumbuka kujitafutia marafiki wengi ni uangamizi wa nafsi yako.

*Wengine wapo radhi waumie lakini wawapendeze wengine ili tu waonekane wapo vizuri hii ndiyo inaitwa  ( ujinga)
-Hawawezi kukubaliana  na ukweli wanapokosolewa kwa sababu wameshajiona wapo kwenye daraja la juu wapo radhi kupingana na ukweli ili tu waonekane washindi , watu wa hivi waepuke wasije kukujeruhi .
- Kumbuka kufanikiwa kwa mjinga kutamuua na anayekataa maonyo anataka kufa.

*Wakiona unawazuia kwenye nafasi zao wapo radhi kutunga maneno na kutengeneza story ili tu uonekane mbaya na wao waonekane wazuri.
- Usiogope kwani kila jambo lina  mwisho wake na mwisho wa ubaya ni aibu.

*Usiogope kusema ukweli wakati  wote  hata kama watu watakuchukia lakini kuna  siku  watakukumbuka.
-Usijifanye kukubaliana na kila kitu kiwe uongo,ujinga,uzushi ili tu kuwapendeza watu .

*Kumbuka hakuna mtu  aliyewahi kusifiwa kwa uongo na unafiki bali mtu husifiwa kwa haki na kweli.

*Hatuna maisha mengine zaidi ya haya tunayoishi hivyo acha kupoteza muda kwa mambo yasiyokusaidia.
-Acha kazi ya mshumaa kumulikia wengine huku Wewe unaendelea kuteketea.
- Ishi maisha yako.
-Kuwa mkweli kwako binafsi na kwa wengine.
-Acha uzushi,uongo na unafiki.
-Fahamu huwezi kufukia nafasi ya mwingine  ata  ukimuua bado damu itazungumza,hivyo usijifanye Wewe ndiyo unajua kila kitu tumia nafasi yako kwa uwezo wako za wengine  waachie wenyewe.

*Usisahau kwamba huwezi kufanya kila kitu na huwezi kumpendeza kila mtu  hivyo fanya sehemu yako na ushukuru Mungu kwa nafasi yako .

Continue Reading...

MAMBO HAYA NI MUHIMU KATIKA MAHUSIANO YOYOTE

No comments:


*Usipokuwa makini  na watu unaohusiana nao kirafiki au kimapenzi  kuna uwezekano mkubwa wakachangia kuinua maono yako au kuyashusha kabisa.

*Kila uhusiano unaojihusisha nao lazima utafanya  kitu kimoja wapo au viwili kati ya hivi:
-Kukuinua
-kukushusha
-kukupoteza

*Uwe makini na watu unaotaka kuhusiana nao au waonataka kuhusiana nawe.
-Siyo wote Unaohusiana nao wanapenda kuona unafanikiwa.
-Watu unaohusiana nao kama hawakupandishi  kimtazamo basi wanakushusha.

*Usilazimishe wakuelewe  kile unachofanya maana pengine hawaoni unachokiona.

-Usiwe mwepesi kuzungumza maono yako kwa kila  aliye  karibu  yako ikiwa hujamuelewa vizuri.

-Wengi walio karibu  nawe hawataki uwazidi, wanataka mfanane.

-Watu wengi walioshindwa na kupoteza maono yao walikatishwa tamaa na watu  wa wakaribu  yao.

*Kumbuka siyo wote wanaotaka kuwa karibu nawe wana malengo mazuri kwako.
-Wengine wanataka  kuiga unachofanya.(kukuzunguka)
-Wengine wanataka kukumaliza.
-Wengine wafaidike na ulicho nacho kikiisha wataondoka(kupe)
-Wanataka  kukujua  kiu ndani(wakuaibishe).

-Wengine wanatafuta  kuchukua nafasi yako.(usaliti).

-Wengine wanataka  waonekane tu wapo na wewe.

*Tafuta kuhusiana na watu unaofanana nao kimtazamo na kitabia.
-Angalia watu waliofanikiwa kama wewe au waliokuzidi .
-Usiangalie tuu muonekano wa mtu  bali angalia maadili aliyo nayo.

Continue Reading...

Wednesday, March 22, 2017

JITAMBUE: FAHAMU MTAZAMO UTAKAOUKUPA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO

No comments:
Tembo wa kufugwa  na fundisho kuhusu mitazamo ya mafanikio

Katika maisha huwa tunapambana na mambo mengi ukiacha ya nje ya sisi wewe kama vile hali ya kiuchumi, elimu na siasa, kuna mapambano ambayo huwa tunayo ndani yetu ambayo bila mtazamo sahihi, kupata mafanikio ni ngumu.
Katika makala hii tutatumia mfano wa tembo wa kufugwa anavyobadilishwa mtazamo na kujiona hana nguvu. Soma vizuri mfano huu ili ujue unajipangaje katika kutumia nguvu zako ambazo leo huzioni hivyo unashindwa kuzitumia fursa zilizopo machoni pako.

Mfano wa tembo wa kufugwa
Tembo ni mnyama mkubwa sana,  anaweza hata kupindua gari, anaweza haribu nyumba na kufanya madhara makubwa tuu akiamua. Hata hivyo si ajabu kukuta tembo akiwa amefungwa kwenye kamti tuu na kamba au mnyororo wa kawaida kiasi kwamba kama akiamua kutumia nguvu zake anaweza kujinasua kutoka hapo alipofungwa.
Hata hivyo tembo wengi wa kufugwa hulazimishwa toka wakiwa wadogo kuamini kuwa wao hawana nguvu ya kujinasua toka sehemu walipofungwa.
Kinachofanyika kwa tembo hawa wa kufugwa ni kuwawekea vizuizi vikali toka wakiwa wadogo kabisa. Wakati huo wadogo kweli watajitahidi kwa nguvu zao kutoroka ila vizuizi wanavyowekewa huwazidi nguvu hivyo hubaki hapo hapo. Masikini tembo hawa hali hiyo huwafanya waamini hata wakiwa wakubwa kuwa hawawezi kujinasua hivyo si ajabu katika sehemu nyingi wanazofuga tembo kwa matumizi binafsi huwa wanaweza kuwafunga tuu tembo kwa mnyonyoro au kamba ambayo inaonekana ni rahisi kutoroka ila tembo hatofanya juhudi yoyote ya kutoroka.
Je wewe nawe ni kama huyo tembo wa kufugwa ?
Kila binadamu ana nguvu kubwa ambayo Mungu kaiweka ndani yake. Hata hivyo pengine wewe hujagundua au kuanza kuzitumia nguvu zilizopo ndani yako kwa sababu kama tembo wa kwenye mfano hapo juu, haujioni kuwa una uwezo wa kufanya hivyo.
*Nimekuambia story hii kwakua kama walivyo tembo, pengine na wewe kuna kitu umeaminishwa kutokana na maisha yako ya hapo kabla.
*Pengine ni kutokana na mazingira uliyokulia, kazi yako, elimu yako, marafiki na mwenza wako katika mapenzi, umekaa ukiamini kuna mambo huwezi kufanya.
*Umeruhusu kutokufanya mambo kwa sababu tuu unadhani huwezi, kwa sababu hapo kabla ulijaribu ukashindwa, kwa sababu watu wengi wamekufanya ujione wewe huwezi.
*Amka leo, jiulize je ni mangapi uliwahi kuwaza huwezi ila leo umeweza ? Kwanini hilo lingine unalosema hauwezi  libaki tuu kuwa haliwezekani ?
*Kumbuka #mafanikio huanza na namna akili yako inavyochukulia mambo. Vile unavyowaza ndivyo utakavyokua. Jione kwanza mshindi, jione kwanza kweli wewe ni wa kufanikiwa.
*Ili uweze kubadili maisha yako, inabidi kwanza wewe mwenyewe ujibadili, na hakuna njia bora ya kujibadili kama kubadili kwanza mitazamo yako haswa mitazamo ya kutokuweza.  
*Kumbuka akili yako ni chombo chenye nguvu sana, anza leo, ijaze akili yako na vitu chanya, ijaze akili yako vitu ambavyo vinawezekana.
Ufanye nini ujikomboe toka minyororo uliyopo ?
Kumbuka kile unachokipa nguvu  katika akili yako, ndicho kitakachokutawala, na ndicho kitakachokufanya uwe vile utakavyokuwa.
Usiogope kwamba watu watakushangaa kwani hawajawahi kuona uwezo wako mkubwa. Sote tuna uwezo mkubwa sana, mara nyingi wengi huwa hawautumii kwakua kama wewe vile umejiona hauwezi.

Continue Reading...

Friday, March 17, 2017

KWANINI MAZOEA HAYA NI ADUI WA MAFANIKIO YAKO

No comments:
tabia_zilizo_adui_wa_mafanikio
Tumekuwa tukifanya mambo kwasababu tumezoea hata kama hatufaidiki tunafanya tu.
Na hii imetukwamisha maeneo mengi kama shuleni,kazini,mahusiano ,biashara, familia na hata kwenye nyumba za ibada.
Katika makala hii tutaangalia mazoea haswa mazoea mabaya yalivyo audi wa mafanikio yako na tutahitimisha kwa kuangalia namna gani unaweza kujikomboa kutokana na mazoea mabaya.

Kwanini ni rahisi kufanya mambo kwa mazoea
Ukishazoea kufanya jambo, basi jambo hilo huwa rahisi kwako kwani unaweza jisikia kama vile ni sehemu ya maisha yako. Jambo jipya ambalo hujalizoea huonekana gumu, na hivyo ni rahisi kwako kuona bora ufanye lililo rahisi yaani lile ulilolizoea.
Na ndio maana unapomwambia mtu inakubidi ubadilishe mfumo uliozoea kuutumia na utumie mbinu mpya kufanikiwa atakwambia siwezi nimeshazoea hata kama hicho kitu kinaathiri maisha yake hajali.
Vitabu vya dini vinasema kuna mtu jeshi lake lilikuwa likipigana vita na akaona usiku unaingia ,na haikuruhusiwa kupigana vita usiku. Akatamka na kusema jua na mwezi visimame navyo vikasimama . Akapigana vita na jeshi lake likashinda, alifanikiwa kwasababu aliona inawezekana kusimamisha mambo mengine hata kama siyo kawaida ili tu ashinde . Siyo kwa sababu ni mazoea usiku umeingia basi ameshindwa,Ila yeye alitafuta kushinda kwa namna yoyote ile ambayo ni halali.

Mazoea yanavyokudanganya
Tatizo la mazoea ni kuwa yanaweza kukufanya uamini kuwa wewe  ndivyo ulivyo hivyo na kuwa huwezi kufanya tofauti na hivyo. Mara ngapi umekua ukisema huwezi kufanya jambo fulani kisa tuu eti wewe upo hivyo. Unakubali kuwa mambo fulani yapo juu ya uwezo wako kwakua tuu hujawahi kufanya hayo mambo na kwamba hayo mambo ni kinyume na mazoea yako.
Angalia mifano hii jinsi mazoea yanavyowafanya watu wasifanikiwe:
-Hata mende wamekushinda akili  na kubaki ndani ya nyumba yako kwa maana wanatawala ndani ya nyumba yako unasema ni kawaida.
-Kucha,meno na vingine vingi umeshindwa kusafisha umeridhika unasema nimeshazoea tu kawaida tu.
-Huwezi mpelekea zawadi mume/mke na ukamkumbatia na kumwambia unampenda sababu umeshamzoea ni wa kawaida.
-Kuna aina fulani za nguo nzuri tu za heshima huwezi vaa sababu umeshazoea kuvaa unavyo vaa.
-Huwezi kufika nyumba ya ibada kwa muda uliopangwa sababu umeshazoea kuchelewa.
-Huwezi kupika chakula kwa namna nyingine kikawa na ladha nzuri zaidi sababu umeshazoea kupika mradi umepika.
- Hata ukisikia kuna mbinu mpya unazoweza kufundishwa kuboresha biashara yako,hutaki kwa sababu umeshazoea tu hivyo na unapata pesa inatosha.
-Unakuta mtu ana uwezo wa kununua anachotaka lakini ni lazima aombe mtu amnunulie kwa sababu ameshazoea kuomba omba.
-Huwezi kubuni kitu chako binafsi sababu umeshazoea kuiga iga.

Hatari Ya Mazoea Mabaya
Angalia Mazoea Yatakukwamisha Mengi katika maisha kama vile:
*Yatakutenga na watu ambao wangekusaidia.
*Yataazuia mafanikio yako.
*Mungu hawezi kukubariki ikiwa unafanya vitu kwa mazoea bila kumaanisha.
*Huwezi kwenda mbali kwa kufanya vitu kwa mazoea.
*Hata afya itakuwa ya mgogoro sababu tu ya mazoea
vunja mazoea na utafute kuwa bora zaidi na kufanya mambo kwa ubora zaidi.

Unaanzaje kubadilika ?
Kama ilivyo mazoea mabaya huwa sehemu ya maisha yetu na kutufanya tujisikie sisi ni kama vile tulizaliwa tupo hivyo, nakualika leo uanze kujizoesha mambo yaliyo bora. Najua kuanza itakua ngumu ila utakapoweza kurudia mara kwa mara basi utaweza kujenga mazoea mazuri na hapo utakua mtu bora.
Tumia uwezo wetu binadamu wa kubadilika na kuzoea mambo kufanya uwe na mazoea mazuri na utafanikiwa.
Kila la kheri. Soma zaidi mambo ya maisha na mafanikio katika ukurasa wetu wa Facebook; www.facebook.com/tutunatablog. Bofya hapa ku like ukurasa wetu.
Continue Reading...

Thursday, March 9, 2017

MAMBO 5 YA KUFAHAMU KABLA NA BAADA YA KUINGIA KATIKA MAPENZI

No comments:


Mambo_ya_kuzingatia_katika_mapenzi
Mafanikio katika mapenzi huhitaji maelewano , uwajibikaji na busara kubwa ili waliopo katika mahusiano waweze kweli kunufaika na penzi lao. Katika Makala hii tutaangalia mambo makuu 5 ambayo yakizingatia na kufanyika kwa ufasaha yanaweza boresha furaha na mafanikio katika mapenzi.
1. Utofauti kati ya  mahusiano, mapenzi na ndoa:
Ni muhimu kwa wapenzi kutambua  kama wanahitajiana, na kama kweli wanataka kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu kabla ya kufikia hatua ya kula kiapo cha ndoa.
Ndoa ni kiapo mbele ya watu wengine , na ni namna ya kutaka kumuhakikishia mwenza wako kuwa endapo kiapo hicho kitatokea kuvunjika, basi unakubali rasmi kuwajibika kwa mujibu wa taratibu zilizopo za ndoa husika, ikiwemo kukubali kuitwa kwenye mabaraza ya usuluhishi, kugawana mali, n.k. Na kwa upande wa kiroho, inabeba maana zaidi kuwa unaweka kiapo kwa Mungu wako kuwa utalinda mahusiano yako na huyo unayemchagua.
Ndoa ni namna tuu ambayo wawili walio kwenye mahusiano wanaamua kuwataarifu rasmi watu wengine kuwa wao wapo rasmi katika mahusiano. 
Hivyo basi, ndoa haijengi mahusiano wala mapenzi. Kiuhalisi inabidi kwanza yawepo mahusiano na mapenzi kisha ndio kiapo kifanyike, kwani kinyume cha hivyo ni kuwa unakula kiapo ‘feki’.
Kutumia ndoa kama kinga ya kuhakikisha mahusiano yako yanadumu ni maamuzi magumu ambayo pengine yanaweza yasilete faida hapo baadae. Au kuingia kwenye ndoa wakati tayari unaona mahusiano yenu tuu ni shida, ila unajiaminisha kuwa mwenza wako kwakua mkiwa kwenye ndoa na kwa sababu ya watoto basi atatulia na mtaishi tuu vizuri ni uamuzi mgumu ambao unawezakana usikuletee mafanikio.

2.Matarajio waliyonayo waliopo katika mapenzi
Kabla hata ya kuingia katika mahusiano na hatimaye ndoa wengi wetu huwa na matarajio binafsi ya kimaisha. Matarajio haya yanajumuisha vile tunavyotaka sie wenyewe kuwa hapo baadae, pamoja na matarajio ya vile tunavyotaka wenza wetu wawe.
Hata hivyo katika hali halisi tunajikuta sisi wenyewe hatuwezi kujibadilisha au kujiweka kwa usahihi vile tunavyotamani kuwa (kwa sababu kwa kila tunachojaribu kufanya kuwa bora, tunajikuta bado tuna madhaifu mawili matatu). Pamoja na ukweli huu wengi hutaka kuwabadili wapenzi wao wawe wa aina fulani hivyo kuishi Maisha ya matarajio ambayo ni magumu wakati mwingine.
Kwakuwa kiasili binadamu ni kiumbe huru, wenza wetu  huwa ‘busy’ kutimiza ndoto za vile wanavyotamani kuwa iwe kimavazi, aina ya marafiki, utafutaji wa kazi , kujiendeleza kimasomo, aina ya mali za kununua, hata kufikiria tofauti aina ya maisha wanayotaka muishi.
Matokeo yake ukinzani huu wa matarajio ni mkanganyiko wa mgongano wa mawazo kati ya wawili nyie, na mwanzo wa vita ya chini kwa chini ya nguvu ya maamuzi katika mahusiano yenu.
Ndio maana sio ajabu kuona wapenzi walioishi pamoja kwa miaka 15 wakiachana kisa ni kuwa mmoja wao amechoka aina fulani ya maisha au ametamani kuwa wa aina Fulani.

3. Kuweza kumbadili tabia mwenza wako
Ni bora uwe na subira uje upate mtu ambaye huhitaji kumbadili tabia au kumtengeneza awe vile unavyotaka wewe kwani unaweza badili muonekano na kumpatia vyote unavyodhani unaweza awe vile utakavyo lakini huwezi kumiliki uhuru wake wa maamuzi na kufikiria. Ipo siku atakuja kubaki yeye kama yeye na kufanya tofauti na vile ulivyokua ukitarajia kwani ulichofanikiwa wewe ni muonekano na kukubaliana kwa maneno na kwa matendo ila kiakili  na kimaamuzi bado kuna bomu linalosubiri kulipuka siku akiamua kuwa yeye kama yeye.
Na la kukumbuka ni kuwa wakati mwingine unaweza usisishinde kumbadili mtu kwakua tayari mtu huyo hajioni kuwa anaweza kubadilika, au ana misingi mingine ya Imani kuhusu hivyo alivyo au anavyopaswa kuwa kiasi kwamba kusikiliza usemacho Hata hivyo wengi wetu kwenye mahusiano, hutegemea ‘mapenzi’au vitisho tuu kama vile ‘nitakuacha mie ’,  kama sababu ya kumfanya mtu abadilike kitabia.Udhaifu wetu katika kutambua asili ya tabia ya mtu husika na mbinu za kisayansi za kubadili tabia hufanya zoezi la kubadilishana tabia kuwa gumu na pengine lisilowezakana.

4. Mtazamo wa kuvumilia katika mahusiano
Kusameheana ni jambo la asili, na tunapaswa kusameheana kwa mambo mengi nje hata ya mahusiano. Hata hivyo msisitizo mkubwa uliopo kuhusu kusameheana katika mahusiano kunafanya wengine waache kujiboresha ili wasikosee na kuwakwaza wenza wao, badala yake wanalalia zaidi katika ukweli kuwa wanatarajia kusamehewa.
Kila mtu analo jukumu la kufanya bidii kuwa mtu mwema, hivyo hauhitaji kubeba ‘uzembe’ wa mwingine kwa kisingizio tuu cha kuwa unaonyesha upendo hususani pale ambapo ni kwa uzembe tuu au kutokujali kwake mwenza husika amefanya jambo fulani.
Amini usiamini, kasumba hii ya kutarajia aina ya pekee ya kusamehewa na kuvumiliwa kwa kisingizio tuu cha kuwa upo kwenye mapenzi na mwenza wako, hurudisha nyuma maendeleo ya mahusiano yenu kwani mwenzi wako nae ni binadamu na kumbuka anayo matarajio mengine ya maisha, isitoshe na yeye anahitaji upendo na kujaliwa na wewe, hivyo kutarajia kwako kusamehewa na kuvumiliwa kunamnyima haki mwenza wako. Hatimaye kutegemea kwako kusamehewa kila wakati, kunamfanya mwenza wako atilie mashaka upendo wako kwake.

5. Uaminifu , Upendo na Kudumu kwa mahusiano
Pamoja na ukweli kuwa mwenza wako anatarajia utakuwa muanifu kwake, elewa kuwa kuwa mwaminifu pekee katika mahusiano yako sio tiketi ya kudumu kwa mahusiano yenu kwakuwa watu wanaingia kwenye mahusiano sio tuu kwa kuwa wanataka kuwa na mtu mmoja muaminifu bali wana mahitaji mengine wanayohitaji.
Zungumza na mwenza wako, fanya utafiti wako binafsi kuhusu mpenzi wako ujue mambo mengine anayohitaji toka kwako. 
Pia msikilize anapokutaka urekebishe mambo kadhaa au ufanye mambo fulani. Inapendeza pale unapomfanyia mtu mambo yanayompendezesha kwa kuwa hivyo ndivyo anavyotaka, sio kwakuwa tuu wewe unadhani kufanya hivyo kutampendezesha mhusika.
Upendo ni kujisikia kujitoa kwa ajili ya mwingine, ni kumfanyia mwenzako vitu anavyohitaji. Usipofanya vitu anavyohitaji ukawa wewe tuu unataka kufanya unavyodhani anahitaji au unavyopenda wewe hapo ni shida. Kumfanya  mwenza wako afurahie uwepo wako kila siku ndio kazi yako kuu katika uhusiano wenu.

Continue Reading...