Sunday, December 11, 2016

MAMBO 4 KILA MWANAUME AYAJUE KUHUSU WANAWAKE KATIKA MAHUSIANO



Wanaume wengi wamekuwa na maswali ni namna gani wanaweza kuwaridhisha wake zao.
Na wengine wamejaribu kuwaridhisha wake zao kwa jinsi wanavyojua wao,ama kwa kusikiliza maneno ya mtaani na kwenye vijiwe wanavyokutana na wakajikuta badala ya kujenga ndoa ndiyo wamepotea kabisa,na badala wake zao wawaheshimu ndio wamewadharau kabisa na kusababisha marumbano na huzuni katika mahusiano.
Hata hivyo ukweli ni kuwa mahusiano ni mazuri na yana raha kama mambo muhimu yakizingatiwa. Ila  kwa wewe mwanaume kama hautofahamu mambo ya msingi kuhusu mwanamke na kuyazingatia unaweza kuchukia mahusiano. Yaani kumbe mahusiano siyo mabaya, ila mbaya ni mwanaume mwenyewe.
Leo tutazungumzia mambo 4 ambayo wanaume wengi hukosea na hivyo kuwafanya wanawake wao waonekane shida katika mahusiano.


Kwanza nikupe habari hii niliyoisikia kuhusu mwanaume mmoja ambaye alikuwa akisema “nimefanya yote ambayo natakiwa kumfanyia mke lakini mwanamke haniheshimu wala hanipendi”.

Akasema “namnunulia nguo,nampa chakula anachohitaji,nawatunza wazazi wake.”

Huyo mwanaume kama walivyo wanaume wengi, kwa upande wake aliona hayo ndiyo mambo muhimu ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwake kama mwanaume na siyo tofauti,na aliona kwa kufanya hayo atakuwa amemridhisha mkewe.
Kumbe hayo mambo hata mwanamke mwenyewe tu anaweza kuyafanya bila mwanaume na kama yangekuwa ni hayo tu basi mungu asingemuumba mwanaume  na mwanamke.


Mambo tunayozungumzia hapa ni mambo ambayo mwanamke anayataka kutoka kwa mwanaume ,ni muhimu mwanaume uyafahamu na utaanza kufurahia mahusiano na ndoa yako.

Kumpenda kwa vitendo na kwa maneno:

Mwonyeshe kwamba unampenda kwa matendo na maneno,unaweza kumpigia, hata vitu vidogo vidogo tuu kama kumpigia simu muda mfupi tu baada ya kuachana na kumwambia jinsi unampenda vinaweza kuwa sehemu ya kuonyesha upendo.

Muonyeshe mahaba:

Wanawake tunapenda kuonyeshwa mahaba kwa kukumbatiwa na kuambiwa vile ambavyo mwanamme anajisikia kuhusu sisi. Mwonyeshe mwanamke kuwa umwambie vile alivyo na umuhimu  na uthamani kwako.

Uwe msikilizaji makini :

Wakati unazungumza naye jambo onyesha kujali,msikilize kwa umakini ukimwangalia machoni. Thamini kile anachokisema na

Mwonyeshe kwamba unamhitaji:

Muonyeshe mwanamke wako kuwa unamhitaji katika maisha yako kwa kumshirikisha katika maamuzi na mambo yako ya msingi. Kama anahitaji kuwezeshwa ili aweze kukusaidia kufanikisha mambo fulani, basi ufanye hivyo. Usimuache mwanamke wako akajisikia mzigo kwako.


Share this article :

7 comments: