Majaribu na matatizo ni sehemu ya maisha ambayo kila aliye hai atapitia. Unapopitia majaribu usidhani upo peke yako, watu wengi wanapitia magumu kuliko yako,sema tu huwafahamu au unawafahamu lakini hujui wanayopitia.
Zingatia yafuatayo ili uweze kushinda magumu na kuwa mwenye furaha:
Usifanye Hali ya Kushindwa ni Yako Peke Yako:
Hebu fikiria mtu mmoja anaposema ameshindwa mara tatu lakini hakukata tamaa akaendelea kujaribu tena na mwingine aseme nilishindwa mara moja na sikujaribu tena.
Kuna uwezekano mkubwa wewe umeshindwa kwa sababu hujataka kujaribu tena,na tunajaribu tena hata tunaposhindwa kwa sababu hakuna mtu aliyeumbwa kushindwa ila majaribu yanapozidi ndio tunafikiri kwamba haiwezekani kushinda.
Changamoto unazopitia siyo mpya wengi wamepitia ila kwako wewe ni mpya.
Kushindwa Leo Haina Maana Kesho Utashindwa Tena:
Je umeshindwa kwenye jambo gani?ndoa,mahusiano,kazi,biashara au huduma?
Usiogope inawezekana tena kushinda ikiwa Mungu amekuacha uishi.
Kila siku ya maisha ni darasa na kila tatizo unalopitia ni mwalimu.
Kushindwa siyo mwisho wa mashindano inategemea unafanya nini kushinda tena.
Usikubali kuishia kushindwa tu.
Fanya Yafuatayo Ili Ushinde Baada ya Kushindwa:
Tambua kushindwa kwako na ukubali yaani jiambie kabisa kuwa ni kweli hapa nimeshindwa na kwanini nimeshindwa.
- Acha kutoa visababu unaposhindwa mfano mimi ni masikini sababu wazazi hawakunisomesha au nimeshindwa mahusiano sababu sina sura nzuri.
- Usiogope kuonekana umeshindwa : Kosa kubwa maishani ni kuishi ukiwa na hofu ya kushindwa tena na kubali kwamba kushindwa ni sehemu ya maisha.
- Kubali kukosolewa na kuelekezwa hivyo basi zingatia haya:
- Usijifanye unajua kila kitu
- Jifunze kwa walioshinda.
- Waza zaidi mbinu mpya za kushinda tena.
- Weka malengo juu ya hicho unachotaka kushinda.
- Heshimu unachofanya na unachosema ili kweli unachopanga kiwe unachofanya.
- Kuwa na msimamo kwa unachofanya.
D. Anza kufanya haya ushinde
- Usipoteze muda na mambo ambayo hayatakusaidia kushinda.
- Usiwaze sana kuhusu mambo yaliyopita.
- Waza kushinda maana walioshindwa maishani walishindwa akilini.
Hitimisho:
Kushindwa ni hali isiyoepukika na kwamba kushindwa mara nyingine ndio njia ya ushindi.
Kila mtu anapenda kushinda katika mambo mbalimbali maishani ila ushindi hautokei kwa bahati mbaya ushindi unaandaliwa. Wanaoshinda hushinda sababu wana mawazo ya kushinda. Jijengee msimamo mzuri na mawazo chanya kuhusu kushindwa kwako, na jipange ili uweze kushinda katika hilo unalotaka kulifanya.
0 comments:
Post a Comment