Kuna
watu wana uchungu mioyoni,wengine wana makovu kabisa kwenye miili yao,wengine
wana vilema vya Maisha. Ukiwasikiliza watakwambia ni marafiki
waliwatendea hayo. Marafiki ni wazuri kama ukimpata rafiki sahihi. Kuna
mtu anaweza kuwa rafiki yako hata watu wanapowaona wanawaona kama ni ndugu na
siyo marafiki tu. Kuna watu wanasema hawataki marafiki marafiki zao
ni wake zao au waume zao ni sawa pia kama unaweza kukaa bila rafiki haina
tatizo.
Hivi unajua kwamba maadui wengi wa watu wametokana na
marafiki yaani kabla hawajakuwa maadui walikuwa marafiki. Pia haya
yanawapata sana wanawake maana wanawake huwa tunafungulia watu mioyo yetu kwa haraka
Zaidi kuliko wanaume. Leo tutaangalia kwa kifupi mambo ya kuzingatia ili
kuchagua rafiki sahihi.
Angalia haya kwa huyo
ambaye ni rafiki yako au unataka awe rafiki yako:
1)Je anaamini kile unachoamini? :-
-Anaamini nini kuhusu ndoa?
-Anaamini nini kuhusu mafanikio ya kiroho na kimwili?
2)Ana mtazamo gani?
-Yeye binafsi anajionaje na anawaonaje watu wengine?
-Kila wakati anapenda kuzungumzia nini?
-Huwa anakuonaje na wewe na anakuwa makini kiasi gani mnapozungumzia jambo flani
linalokuhusu?
3)Ni mtu anayeshaurika?
-Unaweza kumuonywa jambo na akaelewa bila kukasirika?
4)Je ni mkweli?
-Ni mwaminifu?
4)Anaongozana na watu wa aina gani?
Baaada Ya Kufanya Hayo
Baada ya kujiridhisha kwa yote hayo basi sikiliza
moyo wako ukiona unapata amani juu ya huyo rafiki uliye naye au
unataka kuanza urafiki naye .Ila pamoja na hayo yote ambayo utakuwa umejiridhisha
zingatia haya:-
1)Usimwambie kila kitu.
2)Mheshimu.
3)Mpende.
4)Mpongeze anapofanya vizuri.
5)Msaidie na umfundishe pale asipojua.
6)Mpe pole na umtie moyo anapopitia magumu.
7)Shida yake iwe shida yako.
8)Inapotokea mmeshindwa kuelewena katika
jambo flani basi kaeni chini mzunguze yaishe.
Si kweli kwamba hakuna marafiki wa kweli wapo, na
wapo marafiki wanaofaidika na urafiki wao na wanafanya mambo makubwa, hivyo
fanya uchaguzi sahihi.
0 comments:
Post a Comment