Tuesday, December 20, 2016

MAMBO 5 YANAYOWAKERA WANAUME KATIKA MAPENZI



Mapenzi ni matamu lakini yanaweza kuwa machungu endapo hakuna uelewano kati ya hao wapendanao. Namna ya kuchochea maelewano kati ya wapenzi ni kuhakikisha wanafahamiana vizuri na kutimiziana mahitaji. Katika makala hii tutaangalia mambo ambayo wanaume wengi wanalalamika toka kwa wapenzi wao, na ambayo huwafanya wanaume wasifurahie mapenzi na hivyo uhusiano kuyumba.

Mwanamke kukosa imani kwa mwanaume:
Kutokua na imani na mpenzi wako kunatafsirika kama vile kutojiamini wewe mwenyewe. Yupo na wewe sio kwa sababu hakuwaona hao wanawake wengine. Badala ya wewe kumhadaa kwa maneno ya kutomuonyesha unampenda, au kumchunguza chunguza sana, wewe wekeza katika kumpenda kweli kweli, muonyeshe kuwa hajakosea kukuchagua, fahamu anahitaji nini na umpatie vyote. Sio tuu tendo la ndoa, mwanaume anahitaji mambo mengi toka kwako. Je bado anajisikia kuwa wewe ni rafiki yule aliyekua nae wakati mnaanza mahusiano ? Je unaendelea kujipamba na kupendeza kama wakati ule mnaanza mahusiano ?


Mwanamke kutokuwa mshauri na wa karibu :
Biblia inasema mwanamke aliumbwa kama msaidizi wa mwanaume. Wanaume wengi hawapendi mwanamke ambaye sio mshauri. Jitahidi mjenge uwazi na utamaduni wa kuzungumza mambo yenu yawe ya kikazi , kibiashara , mahusiano na watu wengine au familia. Mfahamu vema mpenzi wako na ujitahidi kumpa ushauri kwa hekima na upendo mkubwa.  Kuna wanawake wengine hawajui hata wanaume zao wanafanya kazi gani, hawajui hata magumu wanayopitia na hata marafiki za wapenzi wao.


Mwanamke kupoteza nafasi yake ya umama kwa mwanaume:
Wanaume ni kama watoto wadogo, wanahitaji kujisikia yupo “mama” anayewalinda na kuwafanyia mambo. Ndio maana kwa mfano mwanamme kabla hajaoa na alikua akiishi mwenyewe anaweza kufanya vitu vingi yeye mwenyewe, ila akishaoa tuu hata soksi zake hajui wapi huwa zinakaa.
Hivyo basi usiache kumchukulia mwanaume wako kwa upole kama mmoja wa watoto wako hata kama ni profesa, au ni baunsa. Tambua utahitaji kumsaidia kufanya vitu vingi vidogo vidogo haswa vya nyumbani na vinavyomuhusu yeye mwenyewe. Mfano hakikisha unamkumbusha kunywa dawa kama mgonjwa, kupiga mswaki, kubeba wallet yake, na hata mikutano na dili alizonazo. Mfanye ajisikie ana msaada na mtu anayeweza kumsaidia kweli kweli.


Mtunzie “uanaume” wake:
Wanaume kwa asili yao ni watu wa kutaka kutoa suluhu, ni watu wa kutaka kuwa wa msaada kwa wanawake wao. Wanahitaji kujisikia kuwa wanayo nafasi hiyo na unaheshimu na kuamini kuwa wao wanaweza.  Msifie mwanaume wako kila unapoweza, mshukuru anapokufanyia jambo , muonyeshe kweli unathamini na unajisikia furaha na kujivunia kuwa na mwanaume kama yeye. Usifie wanaume wengi, usimlinganishe mwanaume wako na wanaume wengine, na mwiko kumkashifu, kumsema ua kuonyesha dharau kwake na haswa haswa dharau kwake mbele ya watu wengine. Kuwa makini na utani wako kwake, usipitilize haswa kwa mambo ya msingi. Mfano mwanaume wako mpenzi anakufanyia kitu halafu wewe unaingiza utani kuwa mbona fulani kafanya zaidi kwa mpenzi wake.



Mwanammke kutoonyesha hisia wakati wa tendo la ndoa:
Baadhi ya wanawake hujikuta wanafanya tendo la ndoa na mpenzi kwa sababu tuu ni taratibu  ya maisha au kwa sababu wanadhani ndio jambo ambalo mwanamme analihitaji haswa haswa ni huyo mwanaume afike kileleni yaishe. Hata hivyo kwa mpenzi  wako wa kweli kweli, anahitaji zaidi tuu ya yeye kufika kileleni. Anahitaji akuone na kuhisi kweli kuwa nawe mwanamke unafurahia mapenzi. 

Maoni Yako: Je kwa maoni yako ni yapi huwakera na huwakwaza wanaume katika mahusiano ya mapenzi ? Naomba uache comment yako hapo chini.
Share this article :

1 comments:

  1. Point #1 hapo imenikumbusha msemo unaosema "Men don't trust, Men be trusted"

    ReplyDelete