Thursday, April 26, 2018

UKIFANYA HIVI UTAISHI KWA HASARA.



Kuna watu wanaishi na mpaka watakufa hawajawahi kuishi maisha yao halisi mengi wanayoishi ni ya kuigiza,kuiga,unafiki,kujionyesha na kujifanya wapo  sawa na wanajali zaidi wengine mpaka wanasahau yaliyo ya muhimu  kwao.

*Vizuri kwenda na wakati ila  jaribu  kuangalia jambo hilo  linakusaidia?
-Je  usipolifanya utapungukiwa na nini?
-Je  lina  umuhimu kiasi gani maishani mwako?

*Usifanye kitu sababu wengi wanafanya ili hali  hawajui mwisho wake .
-Usifanye sababu kuna  mtu maarufu anafanya hivyo.
-Usifanye sababu unataka kuwa maarufu umaarufu hautafutwi huwa unakuja wenyewe kwa kutumia ule  uwezo ambao Mungu ameweka ndani yako.

*Kuna  watu wanafanya mambo kwa kuiga mpaka wanatia huruma ili tu waonekane na wao wanafanya kama wengine hata kama hawafurahii wanachofanya hali  hiyo huitwa (unafiki)
- Wengine wanaona wasipokubaliana na mambo yanayoendelea wataonekana siyo wakisasa na labda watakosa marafiki.
-Kumbuka kujitafutia marafiki wengi ni uangamizi wa nafsi yako.

*Wengine wapo radhi waumie lakini wawapendeze wengine ili tu waonekane wapo vizuri hii ndiyo inaitwa  ( ujinga)
-Hawawezi kukubaliana  na ukweli wanapokosolewa kwa sababu wameshajiona wapo kwenye daraja la juu wapo radhi kupingana na ukweli ili tu waonekane washindi , watu wa hivi waepuke wasije kukujeruhi .
- Kumbuka kufanikiwa kwa mjinga kutamuua na anayekataa maonyo anataka kufa.

*Wakiona unawazuia kwenye nafasi zao wapo radhi kutunga maneno na kutengeneza story ili tu uonekane mbaya na wao waonekane wazuri.
- Usiogope kwani kila jambo lina  mwisho wake na mwisho wa ubaya ni aibu.

*Usiogope kusema ukweli wakati  wote  hata kama watu watakuchukia lakini kuna  siku  watakukumbuka.
-Usijifanye kukubaliana na kila kitu kiwe uongo,ujinga,uzushi ili tu kuwapendeza watu .

*Kumbuka hakuna mtu  aliyewahi kusifiwa kwa uongo na unafiki bali mtu husifiwa kwa haki na kweli.

*Hatuna maisha mengine zaidi ya haya tunayoishi hivyo acha kupoteza muda kwa mambo yasiyokusaidia.
-Acha kazi ya mshumaa kumulikia wengine huku Wewe unaendelea kuteketea.
- Ishi maisha yako.
-Kuwa mkweli kwako binafsi na kwa wengine.
-Acha uzushi,uongo na unafiki.
-Fahamu huwezi kufukia nafasi ya mwingine  ata  ukimuua bado damu itazungumza,hivyo usijifanye Wewe ndiyo unajua kila kitu tumia nafasi yako kwa uwezo wako za wengine  waachie wenyewe.

*Usisahau kwamba huwezi kufanya kila kitu na huwezi kumpendeza kila mtu  hivyo fanya sehemu yako na ushukuru Mungu kwa nafasi yako .

Share this article :

0 comments:

Post a Comment