Saturday, December 17, 2016

MAMBO 7 YA KUZINGATIA ILI KUBORESHA MAHUSIANO.


Kila  mtu anayeingia kwenye mahusiano anategemea kupata furaha  na Amani.Lakini inakuwa tofauti na matarajio yao.Amani inawezekana kwenye mahusiano kama mambo muhimu yakizingatiwa.

Kuna vitu visipozingatiwa mwanzo wa mahusiano vitaleta shida badae.Hata unapotaka kujenga nyumba ni lazima uhakikishe msingi umeweka imara huwezi jenga nyumba msingi wa nyumba ya kawaida halafu badae useme  hapana nataka ghorofa haitawezekana kama unataka ghorofa ni lazima ulipe gharama za ghorofa.Ndivyo hivyo ilivyo na mahusiano.

Wengi hulalamika na kusema,mwenzi wangu amebadilika hayupo kama zamani,lakini katika mazungumzo yake unagundua yeye ndiye alianza kubadilika .
Tuangalie basi hapa chini vipengele vya kuzingatia ili kweli mapenzi yawe na furaha na yawe bora kabisa.


Mwanzo  wa Mahusiano
Msidanganyane(a)Mwambie mwenzi wako ukweli.
(b)Mwambie yale unayopenda na usiyopenda.
(c)Kuwa muwazi kwa mwenzi wako.
(d)Onyesha upo tayari kuachana na mambo yote uliyokuwa umeyazoea ambayo kwa sasa yanaweza bomoa uhusiano wenu.

Mfanye Mwenzako Ajisikie ni wa Muhimu
(a)Tenga muda maalumu wa kuwa naye.
(b)Onyesha unafurahia uwepo wake.
(c)Mnapozungumza jambo onyesha umakini kwa kumsikiliza na kuacha kila kitu.
(d)Usijifanye unajua kila kitu na kwamba yeye hajui.
(e)Hata anapokosea mwonye tu na kumuelekeza kwa upendo.

Usifanye Mambo Kwa Mazoea
(a)Kila siku ona ni fursa mpya ya kufanya jambo kwa ajili ya koboresha uhusiano wenu.
(b)Mfanyie jambo jipya ambalo hategemei kwamba utamfanyia.
(c)Usifanye jambo litakalomfanya ajione hana thamani tena kwako.

Usipende Kushikilia Mambo Kwa Mda Mrefu Bila Kusamehe
Anapokosea mweleze kwa upendo na umwambie umemsamehe.
Usiwe mtu wa kurudiarudia mambo kila anapokosea unakusanya makosa anapokosea tena unamkumbusha.

Kumbuka Aliwaacha Wengi Akaamua Kuwa na Wewe
Sasa usijifanye wewe ni mjanja kuliko wote.
Mwonyeshe yeye ni wa kipekee.
Usipende kila wakati kuelezea mambo ya mpenzi wako wa zamani.

Onyesha Hisia Za Kweli Kwake
Kumkumbatia mnapokuwa faragha.
Kumbusu na kumwambia maneno matamu,wengine husema maneno yanayovunja mifupa.
Mfano:Nakupenda wewe tu mpenzi wangu,hakika siwezi kukuacha mpenzi wangu, Unaniweza wewe tu mahabuba.

Mtosheleze
Husika na mahitaji yake ya kimwili na kihisia.
Hakikisha anajisikia vizuri anapokuwa kwa kumtimizia mahitaji yake ambayo una uwezo nayo yale usiyoweza shaurianeni.
Jambo analolipenda lipe kipaumbele.
Tendo la ndoa au mapenzi yafanyike kwa usahihi na kwa kutoshelezana.
“Watu wengi  wakishazoeana tu wakazaa watoto basi wanaona  tendo la ndoa siyo jambo la muhimu ni swala la dharura,na ndio utapata malalamiko mengi kwa wanandoa ama wapenzi wakisema zamani tulikuwa vizuri ila sasa amebadilika.”

Kwa leo tutakomea hapa ,tutaendelea wakati mwingine Mungu akipenda.

Share this article :

1 comments: