Kuna wakati unaweza kuwa unapitia magumu ambayo hakuna anayejua ila wewe na moyo wako tu, hali hiyo inakufanya wakati mwingine usiwe mwenye furaha ,unakuwa na hasira kila wakati ,hujiamini,umwamini mtu ukiona watu wanacheka unahisi unachekwa wewe.
*Inawezekana kinachokunyima amani ni ndoa,kukosa kazi,watoto, mchumba,biashara haina faida,kodi ya nyumba,masomo magumu ,magonjwa ,bosi mkorofi au huduma unayofanya kanisani au msikitini.
*Hicho ni kipande kidogo tu kwenye maisha nacho kitapita,usifikiri hali hiyo unayopitia unapitia mwenyewe ,ni wengi wanapitia magumu tena labda makubwa kuliko yako.
*Tunatofautiana katika kupokea mambo wapo wanaopitia magumu maishani kuliko yako ,lakini wameyapokea kawaida wana amani na maisha yanaenda.
*Vile utapokea tatizo na kuamua kulikuza kuona tatizo ni kubwa kuliko wewe na lina akili kuliko wewe ndivyo litakavyokuwa wakati mwingine unafikiri labda hilo tatizo ni jipya hakuna anayepitia tatizo kama hilo. Kumbe ni vile tu watu hawasemi .
*Acha kuruhusu matatizo yakuongoze na kukutawala,Acha kumwambia kila mtu matatizo yako na uwache kujidanganya kwamba una shida kuliko watu wengine.
*Mungu amempa kila mtu akili na uwezo wa kufanya mambo,ndio tunaona vitabu vya dini vinasema Mungu alimuumba Adamu na Eva lakini hakuna mahali vitabu vinasema Mungu akawatengenezea nyumba alijua amewapa akili ya kuwatosha kufanya mambo na alijua wakinyeshewa na mvua watatumia akili kutafuta njia ya kujikinga ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba.
*Acha kuhuzunika mambo unayopitia ni ya kawaida tumia tu akili yako kufikiri namna unaweza kutatua tatizo lako ukishindwa tafuta wataalamu au watu unaowaona wamefanikiwa katika hilo jambo kutaka ushauri kwao.
*Pia achana na watu watu ambao kila wakati wanasema mambo ni magumu na hayawezekani, kwani kila jambo unalopitia ni size yako unaweza kulitatua ......siunajua mti hulala pale ulipoangukia .... na tatizo ulilonalo unaliweza ndiyo maana limekupata wewe na siyo mwingine. Matatizo tunayopitia maishani yanatufanya tuwe imara zaidi , wewe shahidi hakuna mtoto wa darasa la pili anayepewa mtihani wa darasa la saba ni kitu kisichowezekana ni lazima atapewa mtihani wa kiwango chake alichofikia.
*Pambana kutafuta njia ya kutatua tatizo ulilo nalo usiridhike na kubakia kusema tuu umeshazoea
-Maisha ndivyo yalivyo, au wakati mwingine una acha kutatua tatizo linalokusumbua na unaanza kulaumu.mfano:
-Wazazi,
-Serikali ,
-Mume/mke,
-Watoto au kujihukumu mwenyewe.
SAFARI YA MAFANIKIONI NI SAFARI AMBAYO KILA MTU ALIYE HAI INAMHUSU VIKWAZO NI VINGI NJIANI PAMBANA KUVISHINDA MAANA VIKWAZO VINAINUKA KUTAKA KUKUCHELEWESHA UFIKE KWA KUCHELEWA NA UKATE TAMAA UAMUE KUBAKI HAPO AU URUDI ULIKOTOKA .
0 comments:
Post a Comment