Thursday, February 9, 2017

JINSI YA KUTAMBUA UWEZO MKUBWA ULIOJIFICHA NDANI YAKO


nguvu_binafsi_ya_mtu
Maisha yamejaa kila aina ya changamoto ama wengine husema ni sahani iliyojaa kila aina ya uchafu. Ni wewe kupambana na kutapata kitu kizuri ambacho unakitaka ama kupambana na utoke vile ambavyo Mungu alikusudia uwe. Na wakati mwingine siyo rahisi maana kuna watu wamezaliwa na mpaka watakufa, hawajawahi tumia hata kidogo ule uwezo ambao Mungu ameweka ndani yao.
Mimi huwa ninaamini kila mtu ambaye Mungu ameruhusu awepo duniani  basi Mungu amemuweka kwa kusudi na hakuna aliyekuja duniani kuzurura. Ukitaka kuamini ni kweli fanya uchunguzi, utagundua kuna watu wanao uwezo wa kufanya mambo flani kuliko wengine na ukiwapa kazi nyingine hawawezi ndipo utagundua kila mtu unayemuona yupo duniani Mungu ameweka uwezo tofauti tofauti ndani yakila mtu wa kufanya mambo.
Je unafahamu kuna watu wamezaliwa na watakufa hawajawahi kutumia uwezo nao ukawasaidia au ukawasaidia watu wengine.  Na mara nyingi watu wa aina hii wamekua ni watu wanaolaumu na kutafuta visingizio. Mada hii ni pana sana ila nitaelezea kwa kifupi leo mambo ya kufanya ili ujifahamu na kuanza kutumia uwezo ulio nao.
Mambo ya kuzingatia ili kutumia uwezo ulio nao na ufanikiwe:
1)Jiamini kwamba unaweza na wewe ni wa kipekee;
-Usijidharau wewe ni mtu wa kipekee amini kwamba walioshinda wapo kama tu wewe.
Jiulize je ni mambo gani uliwahi kufanya mazuri na makubwa ?
Je watu wanasema na kukuona wewe unawezasana mambo gani ?
Je ni vitu gani unavyo sasa ambavyo unajua watu wengi hawana mfano familia inayokujali, mahali pa kuishi, kazi, mali fulani,  hata pengine upo katika mahusiano mazuri ya kimapenzi.
Ukitilia maanani katika mambo yako makubwa utajigundua kuwa kumbe una nguvu kubwa na uwezekano wa kufanya mengi mazuri kama hao unaowaona wapo mbali mpaka unajikuta unajidharau wewe mwenyewe.
2)Acha kujilaumu na kulaumu wengine .
-Usipoteze muda kuangalia na kuwaza ni nani alikukwamisha au kujichukia kwasababu haukufanya vizuri.              
3)Anzia hapo ulipo.
-Usiseme nasubiri mpaka mambo yatakapokuwa mazuri ndipo nitaanza kufanya jambo flani.
-Kumbuka mabadiliko hayawezi kutokea yenyewe ni mpaka uyasababishe.
-Hata kama kuna changamoto tumia hizo hizo changamoto kutoka hapo ulipo.
Mfano: Mtu anasema ataanza kufanya biashara mpaka atakapokua na mtaji wa kiasi Fulani.  Anaamini hawezi kuanza na kidogo alicho nacho. Anawaza kikubwa ambacho hana na wala hajui  kwa uhakika atakipata lini hicho kiasi. Ila ukweli ni kuwa mtu huyuo anaweza kabisa kuanza biashara anayotaka kwa kiasi kidogo alicho nacho sasa. Lakini  anatamani kuwa na biashara kubwa kwa haraka kama anavyoona biashara kubwa za watu wengine ila asijue kuwa  walianzia chini labda hata chini Zaidi kuliko uwezo alio nao yeye.
4)Usijifananishe na walio shindwa.
-Kubali unaweza kufanya mambo makubwa Zaidi.
5)Achana na historia yako ya nyuma au ya familia uliyotokea.
-Jione wewe unao uwezo wa kufanya tofauti.
6)Acha kufanya mambo kwa kuiga.
Najua siyo rahisi ila kujiikana na kujitoa kwelikweli ili kufikia maono yako kwa kutumia uwezo ulio nao ndio muhimu.
Pia maisha hayajakamilika kwa mtu yeyote kila siku ni kupambana kuhakikisha unapata kile ambacho hauna ,wewe leo waweza kujiona una shida kuliko watu wote ila kuna watakaokwambia shida zao ukajiona wewe hauna shida. Usisahau pia kwamba marafiki wanaweza kukufanikisha  au kukukwamisha,achana na marafiki wasiokuongeza na kila siku wanakukatisha tamaa .

Share this article :

0 comments:

Post a Comment