Wengine wameishia kujilaumu na kulaumu wengine na kuna watu wamekata
tamaa kabisa ya maisha na kuridhika na hali halisi kusema ni kawaida lakini
siyo kweli.
Matatizo makubwa kwa watu na hata ulimwenguni hayakuanza yakiwa makubwa,yalianza yakiwa
madogo dogo tu na yakapuuzwa, si unajua hata mbuyu ulianza kama mchicha, na
misemo mingi tu kama kama mdharau mwiba mguu huota tende. Ngoja nikuhadithie
kisa kimoja kidogo:
Kulikuwa na shujaa mmoja mwenye nguvu sana.Siku moja katika mizunguko yake akatobolewa na mwiba,alipata maumivu makali sana akakaa chini akautoa.Baada ya kuutoa akashangaa! kamwiba kadogo kamemtesa hivyo , akachukia akaurudishia na kuupigilia kabisa na nyundo.Alifanya hivyo kwa kujiambia hivi, shujaa kama mimi siwezi sumbuliwa na kamwiba kadoogo hivi.Basi siku zikaendelea kwenda mguu ukaendelea kuvimba mwisho mguu ulioza na ikabidi akakatwe mguu.
Hapa tumeweza kuona tu kwa kifupi vile matatizo yanavyoanza na watu wanayapuuza kwa vile wanayaona ni madogo tu na wanafikiri itatokea tu yataisha yenyewe,siyo kweli hakuna tatizo linaweza kuisha lenyewe bila kutafutiwa ufumbuzi na mhusika mwenyewe.
HEBU TUANGALIE MAMBO
YA KUZINGATIA KATIKA KUTATUA TATIZO KABLA HALIJAWA KUBWA
-Ona vile linaweza kuleta madhara makubwa baadae.
-Usijidanganye utavumilia tu jiulize unaweza kuvumilia kwa
muda gani?
-Kubali kuteseka ili tu kumaliza tatizo kabla halijakuwa
kubwa.
-Fikiri vizuri je usipolitatua leo utalitatua lini?
-Watu wanaweza wasikuelewe wakati unapambana kutatua tatizo
dogo leo lakini baadae watakuja kukuelewa.
-Acha kufa na tai shingoni kubali kwamba wewe ni sehemu ya
tatizo na kwamba kulitatua tatizo hilo
ni bora kuliko kujionyesha mshindi wakati kiukweli una tatizo.
NIMALIZIE NA MFANO
HUU.
Mtu anaanza uhusiano na mdada flani ambaye anamuona kabisa
ni mvivu ama ni mchafu ,badala amwambie
mapema kabla hawajaingia kwenye ndoa, eti ananyamaza anasema nikimuoa
atabadilika.Matokeo yake wanaowana ndiyo anakuwa mchafu zaidi tayari tatizo
limeaanza kuwa kubwa,mume anaogopa kuleta hata marafiki zake nyumbani maana ni
aibu. Matokeo yake mume anaanza kulewa na hakuwa mlevi ili tu akirudi asiuone huo
uchafu,mara anatafuta mwanamke mwingine msafi ili ajifariji.
Anaanza kumsema mke wake kwa watu wa nje na marafiki Kwamba
mkewe hafai lakini unashangaa kwanini si alichagua mwenyewe? Si alimpenda
mwenyewe?
Hapo ndio tunarudi na kusema
usidharau tatizo au jambo ambalo unaliona dogo leo limalize mapema ama ujiandae
kabisa kupambana nalo badae kama utaweza.
0 comments:
Post a Comment