Duniani
kuna mambo mengi kuna watu wengi, na kila mtu ana tabia yake tofauti na
mwingine . Tabia hizi za watu tofauti zinaweza kukufurahisha au
kukuchukiza. Na katika kila mazingira
kuna changamoto tofauti tofauti. Siku
zote watakaokuudhi na kukuumiza siyo watu waliopo mbali nawe ila ni wale
utakaokuwa karibu nao. Wale waliokusaidia au uliowasaidia,wanaokujua vizuri na
wewe unawajua vizuri. Hawa ndiyo watu
ambao usipokuwa makini watakuumiza sana na unapoanza jambo ni wepesi kukutia
moyo au kukukatisha tamaa . Waha ndio hutoa pia taarifa zako kwa maadui na
wanafanya hivi maana wanataka uendelee kuwa kama wao.
Tatizo la kutosamehe linaanza kwakua hukutegemea kuumizwa
Kuna watu unawaamini kuwa wanakupenda kweli nawe waamini kwakuwa wanakuchekea. Ila kama ungefunguliwa mioyo
yao usingeamini kama ni wao waliokuwa wakicheka. Ni wepesi sana kujionyesha kwa nje kwamba
wapo nawe bega kwa bega na wanaweza hata kujitolea vitu vingi kwa ajiji
yako,wakati mwingine wanakushauri jambo linakusaidia . Basi unaweka tegemeo
kwao na kuwaamini, wakati umewaamini na unawategemea ndipo unagundua walikuwa wanafiki . Tumeshuhudia watu wachukua maamuzi mabaya
baada ya kugundua walikuwa na marafiki hewa.
Wengine wametengeneza chuki milele wana
huzuni wana uchungu mioyoni mwao.
Hawaamini tena mtu yeyote,wamekuwa na hasira kila wakati. Pamoja na dunia kuwa na watu wabaya ina watu
wazuri, pia kwa hiyo usishindwe kuishi kwa amani kwa sababu ya watu wachache
uliokutana nao maishani.Pamoja na kwamba walikuumiza au waliharibi Maisha yako kabisa ,huna sababu
ya kuwashikilia . Pengine aliyekuumiza
ni mpenzi,mzazi,mtoto au ndugu uliyezaliwa naye.
Zingatia
haya ili uweze kusamehe.
1)Fahamu kwamba kukosea kupo na kama
asingekukosesha huyo labda mtu mwingine tu usiyemjua aweza kukukosea.
2)Wewe pia unaweza kukosea hata kama siyo
kosa kama hilo basi jingine tu.
3)Usipoteze muda mwingi kutafakari jinsi
alivyokukosea ila tafakari,ila fikiri vile unaweza fanikiwa.
Mfano:Mtu amekusema vibaya acha kutafakari
kwa nini aseme hivi? Kwani nimemkosea nini?na maswali mengine mengi kama hayo,
badala yake fikiri namna gani waweza kumuepuka.
4) Usitegemee kuombwa msamaha ndiyo usamehe
,maana kuna wengine hukosea bila kujua kama wamekosea.
Faida
za kusamehe.
1)Unaposhikilia jambo kwa mda mrefu
kichwani utashindwa kufiri vizuri mambo ya msingi,kwa hiyo unaposamehe
unaisaidia akili yako kufikiri mambo kwa wepesi Zaidi.
2)Pia utakuwa na furaha wakati wote maana
hauna jambo linalokupa huzuni kila wakati.
3)Utaheshimika na hawa unaowasamehe na
watakuogopa maana wao walitegemea baada ya kufanya waliyofanya ungenyong’onyea
sana.
Baada
ya kusamehe kumbuka haya yafuatayo:
1)usimwani sana mtu na kumwambia kila kitu chako.
2}Pia siyo lazima baada ya kumsamehe
uhusiano wenu ukawa kama zamani,maana labda hilo jambo alilokukose huyo mtu ndiyo udhaifu wake kwahiyo mnaweza
rudisha uhusiano akarudia tena kukuumiza.
3)Pia siyo wote wanaokosea wamekusudia,kuna
wengine imetokea tu hata kama ni kosa kubwa unaweza kumsamehe na mkaendelea na
ukaribu ikiwa alipokosea alionekana kujutia kosa lake.
Samehe
tu bure ili wakati mwingine na wewe ukikosea usamehewe.
0 comments:
Post a Comment