Mungu amemuumba mwanadamu na kumpa kinywa ili aweze kula chakula aishi na aweze kuwasiliana kupitia kinywa hicho, ila wengi wetu tumekuwa tukitumia tofauti na baadhi wanatumia vizuri.
Yale unayosema yatakutambulisha
wewe ni nani na maneno yako yatakuunganisha na watu wa aina yako.Pia maneno
yako yanaweza kukutenga na watu au kukuunganisha na watu.
Na kuna watu wameshindwa kufanikiwa
sababu ya midomo yao,siyo lazima kuongea ikiwa huna kitu cha kusema. Usiongee
tu sababu unataka kuongea.
Jiulize haya kabla hujaongea;
-kwa nini unataka kusema hayo
unayosema?
-Watu watafaidikaje na hicho
unachosema?
-Watu watakuelewaje baada ya
kukusikia?-
-Je ni muhimu sana kusema hicho
unachosema kwa wakati huo na mazingira hayo?
-Wewe binafsi utapata faida gani na
hicho unachosema?
-Na ukiona haina ulazima wewe
kuongea nyamaza.
-Jiulize mbona wengine hawasemi na wewe
ndio unataka kusema?
Sikia hiki kisa kuna kitu
nataka ujifunze:
Kuna mwanamke mmoja alienda kwa
mganga, akitaka mganga ampe dawa amuwekee mume wake maana mume wake alikuwa
akichelewa kurudi nyumbani,anarudi amelewa na mke anapojaribu kumwambia mbona anafanya
hivyo alikuwa akimpiga.basi mganga akamsikiliza yule mwanamke akagundua yule
mwanamke anaongea sana.
Basi mganga akafikiria ni jinsi
gani ataweza kumsaidia huyu mwanamke ili apunguze maneno mengi ambayo ndiyo
yanampelekea mume wake kurudi usiku,huku amelewa ili asimsikie akiongea.Mganga
akampa yule mwanamke majivu akamwambia hiyo ni dawa,jinsi ya kutumia sasa
akamwambia afanye kazi zake mapema kabisa akimaliza aoge na kujipaka hiyo dawa
kidogo mikononi na usoni kidogo ahakikishe haionekani na amsubiri mumewe,mumewe
anaporudi amkumbatie na ,amshike na ile mikono aliyojipaka dawa na kumbusu na
kumwambia anampenda .Baada ya hapo amtengee maji ya kuoga akimaliza kuoga
basi ampe chakula.Wanapofika kitandani ampe mapenzi motomoto.Na ikiwa
atamwongelesha mumewe maneno mengi au kwa ukali basi dawa ingeharibika.Mwanamke
akafanya kama alivyoagizwa na mganga mume akashangaa mbona mkewe haongei sana
kama mwanzo?siku ya kwanza, ya pili , ya tatu mume akaacha pombe akaanza kuwahi
nyumbani na ndoa ikawa na Amani.Akarudi kumshukuru mganga akamwambia maneno
yake mengi ndiyo yaliyokuwa yakiharibu ndoa yake,basi yule mwanamke akajifunza
kwamba namna gani anafaa kuzungumza na mumewe.
Turudi kwenye mada yetu.
-Siyo lazima useme kila unachokiona
au unachoambiwa au unachosikia.
-Usiseme habari za mtu ambazo
hajakutuma kusema.
-Usifikiri watu walionyamaza
hawazungumzi hovyo labda hawajui unachokijua au hawaoni unachokiona.
-Hakikisha unasikiliza Zaidi
kiliko kusema.
-Usipende kuzungumzia jambo
usilolijua vizuri maana hii itawafanya wanaokusikiliza wakudharau.
-Sema ukweli.
KUMBUKA HII SIKU ZOTE.
Mpumbavu akinyamaza katikati ya
wenye hekima naye huhesabiwa pamoja na wenye hekima.
0 comments:
Post a Comment