Kati ya kitu ambacho kinasumbua wengi na kimekwamisha wengi ni tabia.Wengi wana huzuni ndoa zimewashinda,kazi zimewashinda,fedha na mafanikio vimewakimbia,watoto wamewashinda,hawana marafiki hata miili yao haina afya kwa sababu ya tabia tu.
Wengine wamejiona ni kama wana laana,wengine wanafikiri labda wanaugua ugonjwa flani lakini shida siyo shida nitabia zao tu.
Hebu tuone namna gani tunaweza badilika au kubadilisha tabia zetu.
Tafuta Kujijua Binafsi:
Jiulize kwa nini umekuwa ukikwama mara kwa mara katika eneo flani kama vile:-
(a)Kwanini haudumu ktk mahusiano ya kirafiki au ya
mapenzi.
(b)Kwanini
umeshindwa kufanikiwa kimaisha.
(c)kwanini
watu wanakuchukia.
(d)kwanini
hau-dumu kwenye kazi.
Unaweza pia kumuuliza mtu unaye
mwamini akwambie jinsi ulivyo.Jione Kwamba Unahitaji Kubadili Tabia:
Kubali binafsi kwamba haukuwa ukifanya vizuri kwa kuzingatia yafuatayo:-
(a)Chukia hiyo tabia.
(b)Ona jinsi imekukwamisha mambo mengi.
(c)Usiogope kwamba watu watakucheka au watasemaje sababu hapa unahitaji mabadiliko na ukumbuke ni wewe unaumia na siyo watu.
(d)Hata kama utaumia na kuteseka vumilia tu maana unatengeneza kitu kizuri.
(e)Usiwe mbishi kubali kukosolewa na kuonywa bila kukasirika na usiwe wa kujitetea sana.
(f)Kubali kuambiwa ukweli hata kama unauma na usikasirike.
Chukua Hatua Kubadili Tabia:
Anza kufanya kinyume na ulivyokuwa umezoea kwa maana ya kwamba yale ambayo ni mazuri sasa. Zingatia haya:-
(a)Wataalam wa mambo wanasema ili jambo liwe tabia linafaa kufanya kwa siku “21” bila kuacha baada yah apo jambo hilo litakuwa tabia.
(b)Ikikubidi kubadilisha mazingira ambayo unahisi ndiyo yamekuharibia tabia badisha hata kama itakugharimu.
(c)Ikikubidi kubadili marafiki ambao wamekuwa wakikushauri vibaya achana nao tu utapata marafiki wengine.
Majumuisho
Kumbuka haya:
(a)Tabia inaundwa au inatengenezwa na tabia ya mtu inamtegemea mtu mwenyewe na maamuzi yake.
(b)Tabia yako inaweza kukukwamisha kabisa katika Maisha yako yote au kukufanikisha katika mambo yote.
(d)Tabia yako itakutenga na watu au itakuunganisha na watu.
SASA UAMUZI NI WAKWAKO KUTENGENEZA TABIA YAKO ILI WATOTO WAKO WAIGE MEMA KUTOKA KWAKO.
Wynn Las Vegas vs. Encore Casino - KTNV
ReplyDeleteBoth 시흥 출장마사지 hotels offer some sort of concierge, but each has its own VIP option. In addition, 안성 출장안마 Wynn Las 포천 출장마사지 Vegas offers 여수 출장마사지 complimentary 남원 출장샵 wireless Internet access